|
Moto mkubwa wateketeza mali za watu jijini
2008-05-08 14:38:27
Na Radio One Habari
Moto mkubwa umezuka katika jengo moja la ghorofa linalokaliwa na watu,lililo karibu na msikiti wa Mtoro, Kariakoo jijini Dar es salaam.
Mmiliki wa jingo hilo Bwana Mamstameri Artan amesema moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana, ulianza usiku wa manane.
Juhudi za kuuzima zinaendelea kwa ushirikiano kati ya vikosi vya zimamoto vya manispaa zote za jiji la Dar es salaam, uwanja wa ndege na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ.
Msimamizi wa shughuli za uzimaji, Kamishna wa Kitengo cha Usimamizi wa Vikosi vya Zimamoto nchini Bwana Rogatus Kipali amesema ugumu wa kazi ya kuuzima moto huo umechangiwa na kuwepo kwa bidhaa chini ya jengo hilo ambazo hazipaswi kuwemo humo.
|