09 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

TBL kuanza kuwakopesha wakulima wa shayiri Mbeya
 
2008-05-09 16:41:05
Na Radio One Habari

Kampuni ya Bia Tanzania-TBL- kwa kushirikiana na benki mbalimbali hapa nchini imeanza mchakato wa kuwakopesha wakulima wa mkoa wa Mbeya ili waanze kulima zao la shayiri.

Shayiri hiyo itanunuliwa moja kwa moja katika kampuni hiyo ambayo inatarajia kujenga kiwanda chake hivi karibuni jijini Mbeya.

Mkurugenzi wa Uhusiano na mtaalamu wa Shayiri wa TBL, Bwana Focus Laswai ameiambia Redio One kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utawaongezea uchumi wakazi wa mkoa huo wa Mbeya.

Amesema TBL imelenga kutoa upendeleo wa ajira kwa wakazi wa eneo hilo pindi kiwanda hicho kitakapoanza kazi.

Kiwanda hicho kitakuwa kinahudumia mikoa ya kusini na nchi jirani.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.