|
Wakazi wa Rufiji walipwa fidia kwa mradi wa umeme wa Songas
2008-05-09 16:41:53
Na Radio One Habari
Wakazi wa vijiji viwili vya wilaya ya Rufiji wamelipwa fidia ya mazao na baadhi ya nyumba zao zilizobomolewa ili kupisha mradi wa umeme wa Songas kutoka Songosongo mkoani Lindi.
Wakizungumza na Radio One Stereo wakazi wa vijiji vya Umwe Kaskazini na Mkupuka wameishukuru serikali kwa kuwapatia haki yao.
Akizungumzia suala hilo, Afisa Ardhi wa wilaya ya Rufiji Bwana Leo Rwegasira amesema shilingi milioni 153 zimetolewa na serikali kwa ajili ya kulipa fidia hizo.
Bwana Rwegasira amesema kuwa mpaka sasa kwamba vijiji 14 kati ya 16 tayari vimelipwa na ametoa wito kwa wakazi hao kuwapa ushirikiano wafanyakazi wa mradi huo ili uweze kukamilika mapema.
|