09 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wazazi na walezi hawabanwi na sheria ya kuwaacha watoto kuzurura mitaani
 
2008-05-09 16:42:27
Na Radio One Habari

Wazazi na walezi wanaokimbia majukumu yao na kuwaacha watoto kuzurura mtaani wanafanya hivyo kwa sababu hakuna sheria inayowabana.

Afisa ustawi wa jamii Bibi Beatrice Fungamano amesema hayo wakati akizungumza na shirika la habari la PST katika kituo cha watu wenye shinda mbalimbali cha Nunge wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.

Akisisisita umuhimu wa kuwepo kwa sheria hiyo, amesema kwa sasa kuna idadi kubwa ya watoto wa mtaani, ambayo ni matokeo ya wazazi na walezi kutotimiza majukumu yao ipasavyo na kuwaacha watoto wao wakihangaika mitaani wakijihusisha katika vitendo viovu.

Bi Fungamano amesema baadhi ya watoto wamekuwa wakikimbia makwao baada ya wazazi kufariki dunia na kupata mateso kutoka kwa wanandugu wakiwemo mama wa kambo na wengine kujiingiza kwenye vitendo viovu baada ya kukosa malezi mazuri kutoka kwa ndugu, walezi au wazazi.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.