14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Serikali mkoani Kigoma imekataa kuwapokea raia 181 kutoka Burundi
 
2008-05-14 15:18:34
Na Radio One Habari

Serikali mkoani Kigoma imekataa kuwapokea raia 181 kutoka Burundi waliotaka wapewe hadhi ya ukimbizi baada ya watu hao kuingia nchini na kudai kuwa wamekimbia vita nchini mwao.

Akizungumza na wakimbizi hao katika kituo cha kupokelea wakimbizi katika kijiji cha Kasangezi wilayani Kasulu, mkuu wa mkoa huo Kanal mstaafu Joseph Simbakalia amesema hivi sasa Tanzania haipoikei wakimbizi wapya.

Amesema hivi sasa wakimbizi wote wanarudi kwao kutokana na nchi zao kuwa na amani hivyo hakuna nafasi ya kuwapokea wakimbizi kwa kisingizio cha vita .

Aidha ameamuru kufungwa kwa vituo vyote vya kupokelea wakimbizi Mkoani kigoma na kwamba azma ya serikali ya kuhakikisha wakimbizi wote wanaondoka ifikapo Desemba mwaka huu iko palepale kutokana na kuwepo kwa amani ya kutosha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Burundi.

Wameiambia Radio One Stereo kuwa wamekimbia vita baina ya serikali na waasi wa FNL PALEPEHUTU, ambapo majeshi ya serikali yanawasaka vijijini na kuwaua watu hususani vijana wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa FNL PALEPEHUTU.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.