15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Akinamama wa jijini Mwanza waomba biashara zao ndogondogo kurasmishwa
 
2008-05-15 17:29:02
Na Radio One Habari

Baadhi ya akina mama wanaofanya biashara ndogo ndogo jijini Mwanza wameoimba serikali kutambua na kurasmisha biashara wanazofanya ili kuondokana na usumbufu na hasara wanazopata kutokana na misako ya mara kwa mara ya mgambo wa halmashauri ya jiji hilo.

Wakiongea na Redio One Stereo akina mama hao wamesema wanawake ndio walezi wa familia kutokana na ama kufiwa au kukimbiwa na waume kutokana na hali ngumu ya maisha.

Aidha wameiomba serikali na taasisi za fedha kuwapa mikopo yenye masharti nafuu ili kuinua mitaji yao.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.