15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Toeni taarifa za akina baba wanaowanyang`anya vyandarua-Lusingu
 
2008-05-15 17:29:45
Na Radio One Habari

Akina mama wameshauriwa kutoa taarifa kwa viongozi wa mitaa, kuhusu akina baba wanaowanyang`anya vyandarua na kuvitumia wao, badala akina mama na watoto wao ambao ni waathirika wakubwa wa ugonjwa wa malaria.

Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Dodoma Bwana Wallesy Lusingu ametoa ushauri huowakati akitoa msaada wa vyandarua kwa wakina mama wajawazio, waliojifungua na pia kwa wodi ya watoto, katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.

Amesema, baadhi ya akina baba huwanyang`anya wake zao vyandarua na kuvitumia wao, bila ya kujali madhara makubwa wanayoyapata wakina mama na watoto, wanaposhambuliwa na ugonjwa wa malaria.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Dakta Dausen Kimaro, akipokea msaada huo amelishukuru shirika hilo kwa kutambua uhaba wa vyandarua unaoikabili hospitali hiyo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.