15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kilosa waomba kuianishiwa mipaka ya wakulima na wafugaji
 
2008-05-15 17:35:54
Na Radio One Habari

Wakazi wa wilaya ya Kilosa wameiomba serikali kuainisha mipaka ya ardhi kwa wakulima na wafugaji, ili kuepusha migogoro kati ya makundi hayo.

Wakizungumza na Radio One Sterio wamesema katika baadhi ya vijiji mipaka imefutika hali ambayo inachangia migogoro kati ya wakulima na wafugaji .

Aidha wamelalamika kuwa baadhi ya wafugaji hulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima kutokana na kukosekana kwa maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo.

Wamesema kama serikali haitaweka mipaka huenda yakazuka mapigano baina ya wakulima na wafugaji na wameiomba serikali kutoa elimu ya sheria ya umiliki wa ardhi kwa wakulima na wafugaji wa wilaya hiyo ya Kilosa ili kuepusha migogoroya ardhi isiyokuwa ya lazima.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.