16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Marobota Laki-Moja-Elfu-50- Mia- Sita- 63 ya pamba yameuzwa nje ya nchi mwaka jana
 
2008-05-16 15:46:26
Na Radio One Habari

Marobota Laki-Moja-Elfu-50- Mia- Sita- 63 ya pamba yenye thamani ya zaidi dola za Marekani milioni 43.2 yameuzwa nje ya nchi kuanzia mwezi Julai mwaka jana hadi Aprili 15 mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini Dk. Joe Kabisa ameiambia Radio One Stereo kuwa pamba hiyo imeuzwa katika nchi mbalimbali lakini asilimia kubwa imeuzwa nchi za mashariki ya mbali.

Amesema karibu asilimia 80 ya pamba inayolimwa nchini huuzwa katika soko la dunia ambapo asilimia 60 ya soko hilo ikiwa ni nchi za mashariki ya mbali na asilimia 20 tu huuzwa nchini.

Mkurugenzi huyo amesema katika musimu wa mwaka 2006/2007 marobota Laki Moja Elfu-16 Mia Nne 61 ya pamba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 25.3 yaliuzwa nje ya nchi.

Aidha Dk. Kabisa amesema zaidi ya tani Laki-2 za pamba mbegu zilizalishwa katika msimu wa 2007/2008 na kwamba katika msimu huu uzalishaji unatarajiwa kuongezeka kwa kati ya asilimia 40 na 50.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.