09 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Netiboli Zenji yasaka m.5/-
 
2006-07-09 09:17:53
By Mwandishi Wetu

Chama cha netiboli cha Zanzibar, CHANEZA, kinasaka sh. milioni 5, kwa ajili ya kuendesha kozi ya awali ya waamuzi na makocha wa mchezo huo kwa wilaya zake.

Katibu Mtendaji wa CHANEZA, Sharrifa Khamis ’Sherry’ alisema katikati ya wiki kwa njia ya simu kuwa kozi hiyo itaendeshwa na wakufunzi wenye kutambuliwa na shirikisho la mchezo huo la kimataifa, Restuta Lazaro na Rahima Bakari.

’’Fedha tunazosaka ni kwa ajili ya kusaidia kugharamia kozi yetu, kwa kulipia wakufunzi na shughuli nyingine zote za kozi hiyo,’’ alisema Sherry.

Katika hatua nyingine, Sherry alisema ligi kuu ya Zanzibar inayoshirikisha timu nane za wanawake na nne za wanaume, iliyoanza hivi karibuni, itafikia tamati Julai 29, ambapo mzunguko wa kwanza utamalizika Julai 13 kwenye viwanja vya Gymkhana.

Alizitaja timu za wanawake kuwa ni mabingwa watetezi Jeshi la Kujenga Uchumi, JKU, Mafunzo, Afya, Zimamoto, Bandari, Msambweni, Chipukizi na MTS; wakati za wanaume ni mabingwa watetezi Polisi, Nyuki, JKU na Msambweni.

Alisema timu nne za juu kwa wanawake zitashiriki kwenye ligi ya Muungano, ambayo imepangwa kufanyika Tanzania Bara, kwa kushirikisha pia timu za idadi kama hiyo kutoka Bara.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.