24 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Timu za taifa za vijana kuwa za kudumu
 
2006-12-24 09:22:30
By Bahati Mollel

Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo amesema sasa kutakuwa na wachezaji wa kudumu wa timu za taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17, 20 na 23 baada ya kukamilika kwa matengenezo ya viwanja tofauti vya mazoezi kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Maximo alisema muda mfupi kabla ya kwenda nyumbani kwa mapumziko Krismas na Mwaka Mpya kuwa wachezaji watakuwa wakichezea timu moja kwa muda mrefu na sio kama sasa ambapo anatoka kwenye mashindano ya umri fulani na kuunganisha katika timu nyingine.

’’Hivi viwanja vikikamilika itasadia kuwa na wachezaji wa timu moja bila kunyang’anyana wachezaji, na hii itasaidia hata mchezaji kupumzika. Sio leo yupo katika katika mashindano haya, na kesho anaunganisha yale,’’ alisema Maximo.

Alisema pia itachangia wachezaji kuzoeana na kuweza kucheza kitimu tofauti na sasa waliotoka katika timu za vijana wenye umri chini ya miaka 17 inakuwa vigumu kushika mfumo wa kiuchezaji wa wale waliojiunga nao wa labda miaka 20 au 23.

Aidha Maximo alisema bado anatafuta wachezaji wazuri zaidi wa safu ya kiungo katika Taifa Stars kwasababu bado nafasi hiyo ina matatizo.

’’Tatizo kubwa katika timu yangu ni viungo, wengi ni wakubwa na ndio maana ninaendelea kuwajaribu chipukizi kila mara na watakaocheza vizuri watakuwa na nafasi kubwa ya kucheza mara kwa mara.’’

Alisema kwa sasa wachezaji wote wa Stars wamekuwa wakimuelewa katika mafundisho yake ndio maana walikuwa wakicheza vizuri kwenye mechi za hivi karibuni za kirafiki za kimataifa dhidi ya Angola na JK Congo.

Maximo hajafungwa katika mechi tano, zikiwemo mbili za michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, tangu aanze kuifundisha Taifa Stars Agosti.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.