24 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Dalali amtaka Wambura kuacha kulumbana na Friends of Simba
 
2006-12-24 09:24:09
By Mwandishi Wetu

Wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam wametakiwa kushirikiana katika kipindi hiki cha maandalizi ya michuano ya klabu ya Afrika ili kufanikisha ushindi wa timu yao ya soka.

’’Wanachama wanatakiwa washikamane, wasaidiane na viongozi kwa kila jambo,’’ alisema mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali wakati akizungumza na Lete RAHA jana Jumamosi.

’’Nadhani sasa muda wa malumbano haupo tena kwasababu tayari kuna uongozi madhubuti uliowekwa madarakani kwa matakwa ya hao wanachama wenyewe,’’ alisema Dalali.

Ingawa Dalali hakutaja wazi kuwa malumbano anayozungumzia ni baina ya aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya muda ya Simba Michael Wambura na kundi la wanachama na wapenzi wa klabu hiyo la Friends of Simba, pande hizo mbili ndizo zilizo katika malumbano ya wazi katika siku za karibuni.

Dalali alisema ushirikiano unahitajika kutoka kila pembe hapa nchini ili kufanikisha timu hiyo kuvuka hatua za mwanzo za Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika na kuingia kwenye hatua ya robo fainali, ya ligi.

Wambura amekuwa akiwalaumu Friends of Simba kwa kuhujumu uchezaji wa Simba wakati kundi hilo limetupa lawama upande wa pili likidai kiongozi huyo alikuwa akiwabagua wakati akiwa madarakani kwa kuwa na Simba \’mbuzi\’ na Simba ’kondoo’.

Dalali alisema maandalizi makubwa ya timu hiyo ni muhimu na sasa wamekuwa wakitegemea wanachama mbalimbali, wakiwemo Freinds of Simba, kusaidia kuidhamini katika majukumu mbalimbali ya klabu hiyo.

Mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao yataanza Alhamisi, alisema Dalali na baadaye timu itaondoka Januari 8 kwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi litakaloshirikisha pia timu za Mundu, Miembeni na Malindi.

Simba imepangwa dhidi ya timu isiyofahamika Afrika ya Textile Pangue ya Msumbiji katika raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho ambayo mechi ya awali ya raundi ya awali itachezwa mwishoni mwa mwezi ujao, lakini kama itavuka, itakutana na kigogo Union Douala cha Cameroon katika raundi ya kwanza.

Timu hiyo ya Cameroon imewahi kucheza na Simba mwaka 1979 katika raundi za mwanzoni za Klabu Bingwa ya Afrika ambapo wageni walikishinda kikosi cha kocha marehemu Mansour Magram 4-2 kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya kushinda tena 1-0 nyumbani.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.