24 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mtibwa yakamilisha usajili mchangani
 
2006-12-24 09:24:53
By Bahati Mollel

Baada ya kukamilisha kutafuta wachezaji wenye vipaji timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu inasubiri ratiba ya ligi ndogo itakayotolewa na shirikisho la soka, TFF, ili iweze kuanza mazoezi.

Kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar Salum Mayanga alisema jana Jumamosi kwa njia ya simu kuwa baada ya ratiba hiyo kutoka watapanga programu ya mazoezi kwa kushirikiana na kocha mkuu Mkenya James Siang’a.

Mayanga alisema kwa sasa wamewapa wachezaji mapumziko kwa kuhofia kufanya mazoezi ya muda mrefu, ambayo yangeweza kuleta madhara ya uchovu kwa wachezaji wakati wa mashindano.

’’Sisi tunasubiri ratiba na ikitoka tu, basi tutaanda programu ya mazoezi kwa kuwaita wachezaji wetu na hata wakati huo tutajua ni wachezaji wangapi tuliobaki nao kwa msimu ujao wa ligi,’’ alisema Mayanga.

Alisema kwa sasa Siang’a amekwenda Kenya kwa mapumziko ya sikukuu ya Krismas na atarejea mapema Januari.

Alisema zoezi la usajili wa chipukizi waliloendesha kwa wiki moja kwenye uwanja wa Manungu Turiani, lilikwenda vyema na sasa wanasubiri uongozi wa klabu hiyo inayomilikiwa na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kutoa tamko la idadi kamili ya wachezaji watakaosajiliwa baada ya kubainishwa watakaotemwa, na watakaojiondoa kutokana na kujisajili na timu nyingine.

’’Zoezi lilienda vizuri kwani walikuja wachezaji wengi sana na tumechagua tuliokuwa tukiwataka.

Ila kikosi chetu kitajulikana Januari kwa vile hadi sasa hatujui wachezaji wangapi wataondoka kujuinga na timu nyingine, hivyo wakishaondoka nafasi zao zitajazwa na hawa tuliowachagua,’’ alisema Mayanga.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.