27 Apr 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Polisi wamshukuru Chambua kunusurika
 
2008-04-27 09:59:20
By Mwandishi Wetu

Wachezaji wa Polisi Dodoma wamesema kubaki kwao kwenye ligi kuu ya Bara msimu huu kunatokana na ujuzi wa kocha msaidizi wa zamani wa Yanga na mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Dar es Salaam Sekilojo Chambua ambaye alianza kuifundisha kwenye mzunguko wa pili Januari 26.

Wakati Chambua akiichukua timu hiyo baada ya kutemwa Yanga kufuatia kuajiriwa kwa makocha wawili wa kigeni, Polisi Dodoma ilikuwa kwenye janga la kushuka na ingawa haikutoka katika mazingira hayo, ushindi wa mabao 3-1 Morogoro na sare ya mabao 2-2 na Simba katika mechi mbili ngumu za mwisho vilibakiza.

Wachezaji John Kanakamfumu, Bantu Admin na Mgaza Mhina walisema kwa nyakati tofauti katikati ya wiki kuwa wanampongeza kocha huyo kwa kuweza kuwaweka katika hali bora kimchezo.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.