27 Apr 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mwisho wa Uhuru kucheza Coastal leo?
 
2008-04-27 10:01:08
By Mwandishi Wetu

Uhuru Seleman amesema ataitosa Coastal Union na kujisajili na timu nyingine yoyote msimu ujao endapo timu yake hiyo itashuka kutoka ligi kuu ya Bara baada ya mechi za kilele leo Jumapili.

Akizungumza na Lete RAHA mwishoni mwa wiki Uhuru alisema bado ana ndoto ya Coastal Union kubaki kwenye ligi kuu hasa baada ya ushindi muhimu wa mabao 6-3 dhidi ya Manyema wa Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwa ushindi huo, na ili kubaki kwenye ligi kuu, Coastal ambayo imefikisha pointi 28 na ya tatu kutoka mkiani inalazimika kushinda mchezo wake wa leo Jumapili dhidi ya Ashanti kwenye Uwanja wa Mkwakwani na zaidi.

Mbali na leo kuifunga Ashanti ambayo itakuwa timu ya tatu kushuka daraja baada ya Pan African na Manyema, Coastal itabidi pia iombe Moro United ifungwe katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar ugenini.

Kama Moro United itapata angalau sare, Coastal Union bado italazimika kuomba mambo mengine matatu.

Sare hiyo iwe ya mabao machache, Toto African ifanye maajabu ya kufungwa na Pan nyumbani na yenyewe ishinde kwa tofauti ya angalau mabao matano ili kubaki kwenye ligi kuu.

Uhuru, 21, aliiambia Lete RAHA kuwa ana uhakika wa kuhama kama timu yake itashuka kwasababu klabu kadhaa zimeonyesha nia ya kumsajili msimu ujao, na lengo lake ni kucheza soka ya hadhi ya juu zaidi nchini.

Kocha wa timu ya taifa ya Kenya Jacob `Ghost` Mulee alimuelezea Uhuru, kwa pamoja na Jerry Tegete wa Yanga, kuwa hazina ya soka la baadaye la Tanzania kama watapewa muda baada ya mchezo wa michuano ya Afrika kati ya nchi hizo wiki mbili zilizopita, Dar es Salaam.

``Timu yangu haipo katika nafasi nzuri sana ya kubaki katika ligi kuu. Lakini tunaendelea kuomba Mungu ili tubaki na endapo itashuka basi mimi nitaangalia timu nyingine,`` alisema Uhuru katika kambi ya timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.

Uhuru pia amechaguliwa kwenye timu ya shule ya soka ya Dar es Salaam ambapo wataendelezwa kielimu katika shule ya sekondari ya Jitegemee na baadaye kupelekwa Uingereza katika chuo cha timu ya Bolton Wanderers.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.