04 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Toto washauri
 
2008-05-04 09:29:22
By Mwandishi Wetu

Baada ya kunusurika kushuka kwenye ligi kuu ya Bara, timu iliyopanda daraja mwaka jana ya Toto African imelishauri shirikisho la soka, TFF, kutumia wachezaji wa zamani kama waamuzi ili kupunguza maamuzi mabaya.

Kocha mkuu wa Toto Charles Kilinda alisema mapema wiki hii waamuzi wengi wamechezesha mpira vibaya msimu huu kutokana na wenyewe kutocheza soka kabla.

Kilinda alisema waamuzi wengi waliochezesha mechi za timu yake hawakutoa maamuzi ya haki, walikuwa wenye jazba na hasira na wengine walionyesha dhahiri kutojua wakifanyacho.

``Nilidhani wachezaji wa zamani waliocheza soka ndio wenye kustahili kuwa waamuzi kwani wao soka wanalijua kwa kuwa wamelicheza na hawawezi kutafsiri sheria kutoka kwenye vitabu,`` alisema Kilinda.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.