04 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Makocha Yanga hakuna likizo
 
2008-05-04 09:34:57
By Mwandishi Wetu

Makocha wa mabingwa wapya wa ligi kuu ya soka ya Bara Yanga, Dusan Kondic na msaidizi wake Sokolovski Spaso wamenyimwa likizo na uongozi wa klabu hiyo.

Makocha hao ambao walianza kazi ya kukinoa kikosi cha Yanga mwishoni mwa mwaka jana wamenyimwa likizo ili waendelee na jukumu la kunoa timu kwa ajili ya michuano Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, na Kombe la Tusker itakayofanyika Julai na Agosti nchini.

Habari za kuaminika zilizopatikana kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema makocha hao raia wa Serbia na Macedonia watapewa mapumziko mafupi, badala ya likizo baadaye.

Kwasasa, mwanachama mmoja wa Yanga aliye karibu na uongozi alisema juzi Ijumaa, makocha hao wanaandaa taarifa ya ligi kuu Bara iliyomalizika Jumapili iliyopita.

Mbali na taarifa hiyo, makocha hao pia watatoa mapendekezo ya idadi na umri wa wachezaji wanaotaka wasajiliwe kwa msimu ujao.

``Hawa makocha sasa wapo katika kazi nzito ya kuandaa taarifa na kuweka wazi wachezaji wanaowataka, alisema mwanachama huyo maarufu wa Yanga.

Aidha, mwanachama huyo amesema tofauti na usajili wa miaka iliyopita, Kondic na mwenzake ndiyo ambao wataandaa mikataba ya muda mrefu na mfupi ya wachezaji na kusimamia usajili wao.

``Katika orodha yao wameorodhesha wachezaji wa timu kadhaa za ligi kuu wanaowataka,`` alisema na kueleza zaidi kuwa ``wapo wa kutoka Pan (African), Ashanti United, Manyema na Simba.

``Lakini watakapowasilisha kwa uongozi wataongea nao makocha kwani sio wote wenye kutakiwa na klabu hasa hawa wa Simba.``

Makocha hao wana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.