DP yaishika pabaya Zeco

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Chama hicho, Peter Magwira, alipokuwa akizungumzia hatua ya Tanesco kutoa muda wa siku 14 kwa wadaiwa sugu ikiwa Zeco kulipa madeni yao kabla ya kukatiwa huduma hiyo.

Alisema deni la Zeco la Sh. bilioni 127 ni la muda mrefu na limekuwa likiongezeka badala ya kupungua wakati shirika linakusanya mapato kutoka kwa wateja wake wa Unguja na Pemba.

“Viongozi wa Zeco wajitokeze hadharani waseme kwanini deni limekuwa halilipwi na jitihada gani wamechukua za kupunguza deni, wananchi tufahamu gharama wanazotumia na mapato wanayokusanya kila mwezi,” alisema Mgwira.

Alisema hakuna njia ya kumaliza mvutano wa deni hilo zaidi ya Zeco kulipa kwa sababu Tanesco inahitaji kujiendesha kibiashara ili iweze kutoa huduma bora kwa wateja wake ikiwamo Zanzibar.

"Inasikitisha Zeco wanashindwa kulipa deni wakati hivi karibuni wamepandisha huduma ya umeme kwa wateja wake kwa asilimia 20 ili waweze kumudu gharama za uendeshaji shirika."

"madhara ya kukatiwa umeme ni makubwa kiuchumi, viongozi wa kitaifa wanatakiwa kukaa pamoja kutafuta ufumbuzi wa deni hilo kabla ya Tanesco kukata umeme," alisema.

Magwira alisema kama gharama za kununua umeme kutoka Tanesco ni kubwa, wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme badala ya kutegemea chanzo kimoja kutoka Tanzania Bara.

"Umeme ndiyo injini ya uchumi wa nchi, kama serikali imeamua kukaribisha wawekezaji lazima itafute njia mbadala ya kuwa na vyanzo vingine vya umeme ukiwemo wa upepo au mawimbi ya bahari," alisema.