Zilipotua mil. 50/- za Biko

Droo hiyo ilichezeshwa na mabalozi wa Biko, Kajala Masanja na Mjuni Sylvester 'Mpoki' chini ya uangalizi wa Abdallah Hemed, msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (TGB).

Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles alimpongeza mshindi huyo na kuwataka Watanzania kuendelea kucheza kwa wingi, ili waibuke na ushindi.

Alisema ni furaha ya Biko kuona Watanzania wanaibuka na ushindi, akiamini ni sehemu ya kutoa utajiri kwa watu wanaocheza mchezo huo unaojizolea umaarufu nchini kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha.

Alisema donge hilo ni mbali ya "zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh. 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh. milioni moja zinazolipwa kupitia simu za washiriki".

"Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu kwa kupitia simu za Tigo, Vodacom na Airtel Money, kwa kufanya miamala kuanzia Sh. 1,000 na kuendelea ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na Kumbukumbu ni 2456 huku wanaocheza mara nyingi zaidi wakiwa na nafasi kubwa ya kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na milioni 50 kwa droo za Jumatano na Jumapili."

Biko ni mchezo wa kubahatisha unaojizolea umaarufu mkubwa tangu kuanzishwa kwake huku kwa miezi mitatu ya Mei, Juni na Julai zaidi ya Sh. bilioni mbili zikienda kwa washindi katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.