African Lyon yaingia kambini Zanzibar

Kocha wa Lyon, Ramadhani Aluko ameiambia Lete Raha juzi jioni kwamba na ikiwa huko, timu hiyo itapata mechi kadhaa za kujipima nguvu.

“Tunataka kutumia vizuri kipindi hiki cha wiki ya mwisho ya maandalizi kuelekea Ligi Kuu, tukiamini kabisa tutakuwa na ligi ngumu, ambayo tunahitaji kuwa tumejizatiti ili kuimudu,”alisema Aluko, kocha wa zamani wa Simba SC.

Ikumbukwe, African Lyon timu ya zamani ya mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta itafungua dimba na Azam FC Uwanja wa Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.