Azam nayo kama Yanga kimataifa

Wawakilishi hao wa Tanzania Bara wametolewa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-1, kufuatia ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mechi ya awali jijini Dar es Salaam, mfungaji akiwa Ramadhani Singano 'Messi'.

Azam imeungana na Yanga ambayo juzi ilitolewa katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, lakini mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara watahamia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kucheza mechi moja ya mtoano na timu itakayopangiwa na kisha mshindi atatinga hatua ya makundi.

Wakati huo huo, msafara wa Azam ulioko na timu hiyo jana ulifanyiwa vurugu na mashabiki wa Mbabane Swallows muda mchache kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa marudiano.

Kikosi cha Azam kilichoanza katika mchezo wa jana ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, Erasto Nyoni, Salum Abobakar 'Sureboy', Himid Mao, Yahaya Mohammed, Frank Domayo na Ramadhani Singano 'Messi'.