NIPASHE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (katikati), akilia baada ya kuwakumbuka baadhi ya viongozi waliofariki dunia hivi karibuni. Kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk. Alphonce Chandika na kushoto ni Dk. Anthony Junda, wakijaribu kumtuliza, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kuruhusiwa. PICHA: IBRAHIM JOSEPH

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akizungumza leo na wakurugenzi wa mashirika ya watoa huduma za wasaidizi wa kisheria nchini zaidi ya 200 nchini wakati wa mkutano ulioandaliwa na LSF kwa njia ya mtandao kwa ajili ya kujadili masuala ya kiutendaji katika mradi wa upatikanaji haki nchini ikiwemo utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria kwa makundi yenye uhitaji kwa watu wote hususani wanawake na watoto.