Eshe Buheti: Tumsaidie Ray C

19Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Eshe Buheti: Tumsaidie Ray C

WASANII wameombwa kukaa na kufikiria namna na kumsaidia kwa hali na mali msanii mwenzao, Rehema Chalamila 'Ray C', ili aondokane na matatizo aliyonayo kwa sasa.

Rays C

Aliyeotoa ombi hiyo mwigizaji wa filamu, Eshe Buheti baada ya kumuona Ray C akiwa katika hali mbaya maeneo ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kabla ya kuchukuliwa na polisi.
"Jamani tufanye kitu tumsaidie Ray C, siku zote nilikuwa ninajua anaonewa ila nilichokishuhudia leo nimeumia kutoka moyoni, amedhalilika mwanamke mwenzetu," ameandika Buheti kwenye mtandao wake.

"Nashindwa hata niongee nini jamani, Ray C leo Kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie," alisema.

Video imezagaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Ray C anayedaiwa kuwa ametumia dawa za kulevya, akipiga kelele kwamba anatekwa ilhali alikuwa akipandishwa kwenye gari la polisi.

Top Stories