Akizungumza katika mahafali ya tano shuleni hapo alisema, shule hiyo inapakana na hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro pamoja na eneo la Ambuseli nchini Kenya, wanyama hupita hivyo amezitaka mamlaka husika ikiwemo TAWA kwa kushirikiana na wadau wengine kuweka uzio shuleni hapo.
"Eneo la shule ni kubwa takribani ekari 100, wanyama wana asili ya kufuata ubichi na ukijani mfano tembo, hivyo wanalazimika kuvamia eneo la shule" alidai Lekanet
Mkuu wa Shule ya Sekondari Tingatinga Pantaleo Pareso ameeleza kuwa ukosefu wa uzio katika shule hiyo kumepelekea wanafunzi sita kupata mimba mwaka huu hali iliyosababisha wanafunzi hao kukosa haki yao ya elimu.
Alidai kuwa wazazi wengi wanatumia fursa ya ukosefu wa uzio kama njia ya kuwashawishi watoto wa kike kukataa kusoma, na kukimbilia ndoa na mimba za utotoni na kutaka serikali kuingilia kati jambo hili.
"Jamii suala la elimu ni gumu, watoto wa kike wanalazimishwa kuolewa, kwa mwaka huu tayari wanafunzi sita wanamimba " alieleza Paresso
Hata hivyo alieleza kuwa tatizo la ukosefu wa uzio kumepelekea watumishi wa shule hiyo kuwa na hofu na maisha yao kwani wanyama aina ya tembo na mbogo wamekua wakizurura shuleni hapo, hivyo wamekua wakiogopa kupita usiku kukagua maeneo ya shule na usalama wa wanafunzi.
"Wanafunzi wanatoroka usiku kwenda mtaani, walimu wanahitaji kupitia usiku kukagua usalama wa watoto wanashindwa mazingira si rafiki wanyama wamekua tishio" alisema Pareso.
Akitolea mfano wa kifo cha mwanafunzi wa shule ya msingi Tingatinga 29 machi 2013 aliyeuwawa na tembo, alisema hali hiyo inajenga hofu ,hivyo ni muhimu maeneo ya shule yakawekwa uzio.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema shule hiyo inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa uzio lakini watakacho hitaji nikujuwa gharama nikiasi gani na ukubwa wa eneo ni kiasi gani ili waanze ujenzi mwezi wa kwanza .
"Na waomba wananchi mniachie swala hili nitashirikiana pamoja na EWMA na wadau wengine kuondoa tatizo hili" aliomba Mwaisumbe
Amesema shule hiyo ni miongoni mwa shule za sekondari tisa zilizopo wilayani hapa ,na ni shule iliyopo ndani ja jumuiya ya hifadhi ya wananyamapori Enduiment (EWAM),inayoundwa na vijiji 11 kata nne zilizopo Tarafa ya Enduiment.