NIPASHE JUMAPILI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Hesabu za Serikali (PAC),Naghenjwa Kaboyoka (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Viongozi wa OSHA wakati mafunzo ya usalama na afya yaliyotolewa na OSHA kwa Kamati hiyo ambayo yalienda sambamba na zoezi la ukaguzi wa jengo jipya la Ofisi za OSHA jijini Dodoma. Aliokaa nao meza kuu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya OSHA, Dk. Adelhelm Meru na Mtendaji Mkuu wa OSHA,Khadija Mwenda.

Bilionea mpya wa madini ya Tanzanite, Anselim Kawishe (katikati), akiwa ameshika madini yake yenye thamani ya Sh. bilioni 2.245 Mji Mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara jana. Kulia ni Waziri wa Madini, Dotto Biteko na (kushoto) ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Florens Luoga. PICHA: GIFT

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (Kulia) akisalimiana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mohamed Mchengerwa wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja Ofisa Mkuu wa Uendeshaji Benki ya NBC, Alelio Lowassa (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu.