NIPASHE

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akiipongeza Vodacom Tanzania baada ya kupata maelezo ya vifaa vya kudhibiti mwendo na ajali vinavyofungwa kwenye magari ya wafanyakazi kutoka kwa Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kushoto), alipotembelea banda la kampuni hiyo,wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. Wakifuatilia maelezo hayo, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Adam Malima, na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camilius Wambura.