NIPASHE

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza na mfanyabiashara wa vitambaa, Juma Hamad (kulia), walipokuwa wakitembea mitaani kuinadi Kampeni ya Teleza Kidijitali kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika Tawi la Benki ya NMB Tandika jana. Katika kampeni hiyo wafanyakazi wa NMB walitembea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Namba na NMB Pesa Wakala na kufungua akaunti. PICHA: MPIGAPICHA WETU

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dk. Maduhu Kazi (kulia), akijadiliana jambo na viongozi, wawakilishi wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Norway na Uingereza baada ya mkutano uliowaleta pamoja watendaji wa taasisi za serikali na ujumbe wa wawekezaji na wafanyabiashara 37 kutoka nchini za Norway na Uingereza ulioratibiwa na Norwegian-African Business Association na Kampuni ya Invest Africa kwa kushirikiana na TIC. PICHA: MPIGAPICHA WETU