Tambwe ampa 'hat-trick' mchumba wake

25Jan 2016
Adam Fungamwango
Sema Usikike
Tambwe ampa 'hat-trick' mchumba wake

STRAIKA wa Yanga anaeongoza kwa ufungaji bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Amissi Tambwe amesema 'hat-trick' aliyofunga dhidi ya Majimaji ya Songea ni zawadi kwa mchumba wake, huku akitamba kuwa ataendelea kufunga kila atakapopata nafasi kwa sababu ndiyo kazi yake.

Amis Tambwe (kulia) akipokea mpira kutoka kwa Simon Mbelwa baada ya kufunga 'hat trick'

kuwa magoli hayo aliyofunga Alhamisi iliyopita Uwanja wa Taofa jijini Dar es Salaam ni maalum kwa ajili ya mchumba wake ambaye hata hivyo hakumtaja jina.
"Nashukuru Mungu kwa ushirikiano wanaonipa wachezaji wenzangu unaoniwezesha kufunga 'hat-trick' kwa mara nyingine tena," alisema na kuongeza kuwa kwa sasa hajui kama amefunga 'hat-trick' ngapi tangu aanze kucheza soka Tanzania, ila alisema kazi yake siyo kuhesabu hela bali ni kufunga tu na ataendelea kufunga kila atakapopata nafasi.
Hii ni hat-trick yangu ya pili kufunga kwa msimu huu, ya kwanza nilifunga Desemba 19 mwaka jana wakati Yanga ikishinda bao 4-0 dhidi ya Stand United.
Straika huyo hatari kutoka Burundi anaendelea kuongoza akiwa na magoli 13 sasa, huku akisema lengo lake ni kuvunja rekodi yake mwenyewe ya kupachika mabao zaidim ya 19 aliyofunga msimu wa 2013/14 wakati huo akiichezea Simba.