TANAPA yapata dawa migogoro kati ya wafugaji na Hifadhi ya Ruaha

By Nebart Msokwa , Nipashe Jumapili
Published at 12:01 PM Sep 15 2024
TANAPA yapata dawa migogoro kati ya wafugaji na Hifadhi ya Ruaha
Picha:Mpigapicha Wetu
TANAPA yapata dawa migogoro kati ya wafugaji na Hifadhi ya Ruaha

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA), limeanzisha mkakati mpya wa kutatua migogoro kati ya wafugaji na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kukaa vikao vya pamoja kati ya maofisa wa hifadhi hiyo, wafungaji na viongozi wa serikali kuhusu namna ya kutatua migogoro hiyo.

Vikao hivyo vilianza kufanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za TANAPA Kanda ya Kusini zilizopo wilayani Mbarali ambapo washiriki wa kikao hicho walikuwa ni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbarali, wawakilishi wa wafugaji, maofisa wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Washiriki wengine walikuwa ni maofisa wa TANAPA Kanda ya Kusini na maofisa watendaji wa Kata 11 zinazopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo inadaiwa kuwa ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika.

TANAPA