KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amechangia Sh. milioni 1.1, kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), mtaa wa Ihami usharika wa Ikwete, Jimbo la Makambako mkoani Njombe.
Wakati akichangia kiasi hicho cha fedha, viongozi wengine wa chama hicho, Mwenyekiti wa chama Masoud Othman Masoud aliyeahidi kuchangia Sh. milioni mbili, Kiongozi wa mstaafu Zitto Kabwe Sh. milioni moja na katibu mkuu Ado Shaibu Sh.milioni moja.
Dorothy ambaye alikuwa mgeni rasmi, alichangia fedha hizo juzi, wakati akiendesha harambee ya kuchangia Sh. milioni 13,360,000 zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
Katika harambee hiyo, michango kutoka kwa waumini waliokuwapo katika tukio hilo, ilikuwa ni fedha taslimu Sh. 1.3, huku ahadi ikiwa ni shilingi 60,000.
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kusini, Grayson Shilongoji, ameshukuru ushiriki wao, katika harambe hiyo na kuwaomba waendelee na moyo huo kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada.
"Kiasi cha fedha tunachotafuta ni Sh. milioni 13,360,000, lakini mwanzo huu si haba, ila ninawaombea muendelee na moyo huo wa kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada," amesema Shilongoji
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED