Aweso afanya mazungumzo na Benki ya Exim ya Korea, anadi miradi ya maji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:20 PM Dec 07 2024
Aweso afanya mazungumzo 
na Benki ya Exim ya Korea,
 anadi miradi ya maji
Picha:Mpigapicha Wetu
Aweso afanya mazungumzo na Benki ya Exim ya Korea, anadi miradi ya maji

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametembelea na kufanya mazungumzo na Benki ya Exim ya Korea ambayo ilitoa fedha za utekelezaji wa miradi ya majitaka nchini Tanzania yenye jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 248.3 (Dar es Salaam 90 $US milioni, Dodoma 70 $US million; na Iringa 88.3 $US million).

Aidha, Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na Mifuko mingine Serikali ya Korea itaendelea kuisapoti Serikali ya Tanzania kupitia Sekta ya Maji katika uwekezaji zaidi wa utejelezaji wa Miradi ya Maji.

Utelezaji wa miradi hiyo utaimarisha huduma za usafi wa mazingira, kuondoa na kutibu majitaka. Vilevile, Tanzania imepata msaada wa Dola za Kimarekani milioni 8 ambazo zitajenga mfumo wa kusimamia huduma za maji (Smart Water Management System) katika Mamlaka ya Maji Iringa kutoka Korea Environmental Industry and Technology Institute (KEITI). 

Pia, Kupitia mfumo huo, IRUWASA itakuwa Mamlaka ya Maji ya kwanza nchi kutumia mfumo huo ambao utaongeza ufanisi katika kudhibiti upotevu wa maji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha huduma ya maji. 

Kupitia ziara hiyo, Aweso ameimarisha ushirikiano na wadau wa maji nchini Korea ambao ni K-Water na makampuni mbalimbali hali ambayo imefungua fursa zaidi za kushirikiana katika majengea uwezo watumishi na Taasisi za Maji ikiwa ni pamoja na kuandaa miradi na kutafuta fedha.