Prof. Penina asisitiza wanatamthilia kuwasilisha miswada tuzo Mwl Nyerere

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 05:57 PM Dec 10 2024
Mwenyekiti wa Bodi ya Tuzo za Taifa za Uandishi Bunifu za Mwalimu Nyerere, Prof. Penina Mlama (kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)  Dk. Aneth Komba (kulia).
Picha: Maulid Mmbaga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tuzo za Taifa za Uandishi Bunifu za Mwalimu Nyerere, Prof. Penina Mlama (kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dk. Aneth Komba (kulia).

MWENYEKITI wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Uandishi Bunifu ya Mwalimu Nyerere Prof. Penina Mlama, ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kuwasilisha miswada ya tamthilia ili kushindania tuzo hiyo, akieleza kwamba kasi ya uwasilishaji miswada katika kipenhele hicho bado hairidhishi.

Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam Prof. Penina, amesema uchache wa miswada iliyowasilishwa katika kipengele hicho ni jambo lililowashangaza kwasababu anajua sekta ya tamthilia inawatu wengi lakini hawajaitilia maanani.
 
Amesema akiwa kama mdau wa tamthilia, itakuwa ni jambo la kusikitisha kama itafika mahali mwaka huu kusiwe na mawasilisho ya tamthilia, na zawadi zisitolewe, akisisitiza watanzania wanaojihusisha na uandishi bunifu katika sekta hiyo.
 
“Nitoe ombi kwa niaba ya bodi ya tuzo, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Bodi ya Filamu, mjitahidi tupate mawasilisho katika sekta hii ya tamthilia kwasababu ndio mwanzo mwaka huu tumeingiza kipengele hicho isije ikaonekana kwamba hakuna haja ya kuingiza tamthilia,” amesisitiza Prof. Penina.
 

1

Ameongeza kuwa katika tuzo hiyo mwaka huu wameongeza kipengele cha tamthilia za jukwaani, redio na runinga, akieleza kwamba kuna uhitaji mkubwa sana wa kuendeleza tamthilia zenye vionjo vya kitanzania.

Amesema hivi sasa kwenye runinga watu wengi wanaangalia tamthilia za runinga za kutoka mataifa mengine kama Korea na Uturuki, akisisitiza kwamba tuzo hiyo inalengo la kuleta uwezekano wa kuongeza idadi ya thamthilia ambazo niza ndani zinzoendesha utamaduni wa Tanzania.

“Tunao uwezo wa kutunga na kuonyesha tamthilia ambazo zinaenda sawa na utamaduni wetu na tusiweke utegemezi kila wakati kuleta tamthilia kutoka nje, na katika kila nyanja nne mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Sh. milioni 10, mswada wake utachapishwa kwa gharama za serikali na kusambazwa nchini kote,” amesema Prof. Penina.
2