RAIS Samia Suluhu Hassan amekemea vikali kauli za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya balozi za kigeni kutoka baada ya kutokea mwa kifo cha mwanachama wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ali Kibao.
Akizungumza kwenye hafla ya kufunga mkutano wa mwaka wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi, ambayo pia iliadhimisha miaka 60 ya Jeshi hilo.
Amesema Rais Samia aliweka wazi kuwa Tanzania ni nchi inayojitegemea na yenye hadhi na hivyo haiwezi kuamriwa na watu wa nje kuhusu jinsi ya kuendesha masuala yake ya ndani.
Rais alikemea kauli za kibaguzi zilizotolewa na baadhi ya balozi za kigeni baada ya kifo cha Kibao. Kauli hizo hazikutolewa kwa ridhaa ya serikali za balozi hizo.
Amesema balozi hizo zinapaswa kuheshimu mamlaka ya Tanzania kama vile balozi zetu zinavyoheshimu mamlaka za nchi nyingine hawataruhusu kamwe mataifa ya nje kuwaamulia.
Aidha, Rais Samia alitoa wito kwa vyama vya siasa nchini kuheshimu falsafa yake ya 4R’s ambazo ni Maridhiano, uvumilivu, haki na uwajibikaji na kutochukulia kimzaha uhuru wa kisiasa wanaoufurahia sasa.
Amesema uhuru huu wa kisiasa umepatikana kwa jitihada kubwa, hivyo ni muhimu kuutumia kwa busara, si kwa kuchochea vurugu na machafuko.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED