"Sitaomba radhi, CUF inakufa kweli"- Ado

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:13 PM Sep 18 2024
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu.
Picha:Mtandao
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu.

"Nimesoma tamko la CUF kunitaka kuomba radhi kwa kauli yangu kuwa CUF inakufa na kuwataka wanachama na viongozi wake waliosalia ambao wana moyo wa mapambano kujiunga na ACT Wazalendo. Msimamo wangu ni kuwa sitaomba radhi kwa kauli yangu"- Ado

"Kazi ya siasa ni kazi ya ushawishi. Ushawishi unafanywa kwa hoja sio matusi wala vitisho. Tamko la CUF lililotolewa na Mkurugenzi wake wa Habari ni ishara ya wazi ya Taasisi inayokata roho. Hakuna Taasisi makini ingeruhusu tamko lililosheheni matusi kama lile litoke kwa umma"-Ado

"Binafsi sitaacha kuwashawishi wanachama wa CUF kuja ACT Wazalendo kama ambavyo ninafanya kwa wanachama wa CCM, Chadema, wasio na vyama nk. Hiyo ndio kazi ya mwanasiasa. Badala ya kutoa matusi na vitisho, CUF pia wana wajibu wa kufanya hivyo" Ado

"Ninarejea ujumbe wangu kwa wanachama na viongozi  wote wa CUF wenye nia ya dhati ya kuendeleza mapambano ya kupigania demokrasia: CUF inakata roho, karibuni ACT Wazalendo " Ado

CUF