Waelimisheni wafanyabiashara juu ya umuhimu wa vibali- SP Kidiku

By Rashid Nchimbi , Nipashe
Published at 04:04 PM Jul 22 2024
Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Tanzania, Mrakibu wa Polisi (SP) Suzana Kidiku.
Picha: Polisi Monduli
Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Tanzania, Mrakibu wa Polisi (SP) Suzana Kidiku.

Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Tanzania, Mrakibu wa Polisi (SP) Suzana Kidiku, ametoa maelekezo kwa wakaguzi wa kata za Wilaya ya Monduli kutoa elimu juu ya usafirishaji sahihi wa mifugo.

Amesema kuna baadhi ya wafanyabishara na wafugaji wamekuwa wakikiuka taratibu kwa kutofahamu sheria, hivyo wanatakiwa wapewe elimu ili waweze kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwa na vibali halali pindi wanaposafirisha mifugo yao au kuuza ili mapato ya nchi yasipotee.

SP. Kidiku, kwa kushirikiana na Mkuu wa Upelelezi wa Kikosi hicho ASP. Winbritha Moshi, mapema leo wametoa mafunzo ya sheria mbalimbali zinazohusiana na usimamizi wa mifugo ili wakaguzi na askari kwa ujumla wawe na uelewa mpana.

Amesema kikosi hicho kimeona umuhimu wa wakaguzi hao kupata elimu hiyo ili na wao waweze kuelimisha wananchi kupitia kata zao hali ambayo itasaidia kupunguza makosa ya kiuhalifu.

Aidha SP. Kidiku amemalizia kwa kusema kwamba elimu na uwepo wa ukaguzi wa vibali hivyo utasaidia kupunguza uhalifu wa mifugo kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Marcel Alute toka Kata ya Monduli juu, amesema elimu waliyoipata imewaongezea maarifa katika utendaji wao wa kazi kwani hapo awali kuna baadhi ya sheria na taratibu walikuwa hawazifahamu vema.

Mkuu wa Upelelezi wa Kikosi hicho ASP. Winbritha Moshi.