Arsenal wapingwa Burnley, Man U v Derby FA

13Jan 2016
Lete Raha
Arsenal wapingwa Burnley, Man U v Derby FA

MABINGWA watetezi, Arsenal, watakuwa nyumbani dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza ya Burnley katika mechi yao ya raundi ya nne ya Kombe la FA kufuatia 'droo' ya ratiba ambayo miamba mingi imeepuka timu kubwa.

Baadhi ya wachezaji wa Arsenal

Kikosi cha Arsene Wenger, kinachowania kuwa timu ya kwanza kutwaa kombe hilo mara tatu mfululizo tangu Blackburn Rovers katika karne ya 19, watakuwa na hofu ndogo ya kushangazwa katika mechi yao.
Crystal Palace nyumbani dhidi ya Stoke City ndiyo ratiba pekee iliyozikutanisha timu za Ligi Kuu tupu, ingawa Liverpool itawavaa West Ham United kwenye Uwanja wa Anfield kama kikosi hicho cha Jurgen Klopp kitaitoa Exeter City katika mechi yao ya marudiano kufuatia sare ya 2-2 Ijumaa.
Mechi hizo zitachezwa kati ya Jan 29 na Feb 1.
Matajiri Manchester City wataenda ugenini dhidi ya washindi wa pili wa mwaka jana Aston Villa, ambao wako mkiani mwa ligi, au timu ya daraja la tatu ya Wycombe Wanderers kutegemeana na matokeo ya mechi yao ya marudiano.
Kikosi cha Louis Van Gaal cha Manchester United kitasafiri kwenda kwa timu ya Daraja la Kwanza ya Derby County.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Chelsea, ambao pia ni mabingwa mara nne wa Kombe la FA, pia wanasubiri mechi ya marudiano kujua kama wataenda kuivaa timu ya daraja la tatu ya Northampton Town ya Daraja la Kwanza ya Milton Keynes Dons.

Habari Kubwa