Asasi zafagilia uchumi usio tegemezi

16Sep 2020
Christina Mwakangale
Dar es Salaam
Nipashe
Asasi zafagilia uchumi usio tegemezi

ASASI za kiraia zimesema kuwa ipo haja ya jamii husasani kizazi kijacho, kujiandaa na uchumi usiokuwa tegemezi katika kujiletea maendeleo yao na taifa.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa MediaSpace, Vicensia Fuko, wakati akifungua mkutano ulioshirikisha asasi za kiraia, waandishi wa habari na wataalamu takwimu mtandaoni, jijini Dar es Salaam.

Alisema lengo la mkutano huo ni kupata mrejesho kutoka kwa asasi saba ambazo zilichaguliwa kushiriki katika mchakato ‘StoryTellingChallenge’ ambao ulikuwa ni maalumu kwa asasi hizo kutoa elimu kupitia vyombo vya habari.

Fuko alisema kuwa ili jami kuondokana na umaskini ni wakati sasa wa serikali, kuwa mtaala maalumu wa kuwaandaa watoto kujitegemea kiuchumi.

“Sera ya kujitegemea inaweza kujengwa kwa watoto wetu ili kuondokana na dhana ya kutegemea kutoka kwa mtu. Hii itasaidia kupunguza utegemezi wa kiuchumi kutoka nje,” alisema Fuko.

Alisema kwa sasa inaweza kuchukua muda katika maamdalizi ya nchi kuwa na uchumi unaojitegemea na kusema jamii ianze kujiandaa kisaikolojia.F

Fukoalisema kuwa mchakato huo ulilenga kutoa fursa kwa jamii ambazo zinafanya vizuri katika jamii na zinakosa jukwaa la kuelezea shughuli zao.

“Katika jamii kupitia ulimwengu huu wa mitandao pamoja na baadhi ya watu kutumia vibaya mitandao, lakini kuna asasi za kijamii ambazo wanafanya kazi nzuri lakini hawasiki ,platform’ ni ndogo.

MediaSpace tukaanzisha mradi huu ambao umesaidia asasi kufikisha ujumbe kupitia vyombo vya habari," alisema Fuko.

Mkurugenzi Mtendaji Shirika la ELIMISHA, Festo Sikagonano alisema ushiriki wa asasi hiyo katika mchakato huo, umesaidia kupanua wigo wa shughuli zao kuelimisha jamii kutunza  akiba katika kipato wanachoingiza kila siku.

“Kila familia, au kila mmoja lazima uwe na bajeti ambayo unajua fedha fulani nitafanyia jambo hili la maendeleo, bila bajeti ni sawa na kukimbia bila kujua unakoelekea,” alisema Sikagonamo.

Habari Kubwa