Ndege ya Jeshi iliyotoweka Jumatatu imekutwa majini

13Dec 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ndege ya Jeshi iliyotoweka Jumatatu imekutwa majini
  • Nchi tano zatinga kusaidia

MABAKI ya ndege ya kijeshi ya Chile iliyotoweka siku ya Jumatatu wiki hii, yameonekana juzi.

Picha ya ndege ya mizigo ya kijeshi muda mfupi kabla ya kutoweka. PICHA: MTANDAO.

Maofisa wa Jeshi la Chile, wanasema wamezuia mabaki yanayoaminika kutoka katika ndege hiyo ya kijeshi na yalipatikana yakielea umbali wa kilomita 30 kutoka eneo walilokuwa na mawasiliano ya mwisho.

Vifusi hivyo vilipatikana katika maji yanayojulikana kama mkondo wa Drake. Ndege hiyo ilikuwa inatoka katika mji wa Kusini mwa Chile - Punta Arenas, ikielekea kambi ya kijeshi ya Antarctica, alikokuwapo Rais Eduardo Frei Montalva.

Vifusi hivyo vinasadikiwa huenda vinatoka katika tangi la mafuta ya ndege hiyo, kwa mujibu wa Kamanda wa Wanahewa wa jeshi la nchi hiyo, Eduardo Mosqueira, alipozungumza na wanahabari juzi, kuhusu tukio hilo.

Anasema, Kikosi cha Wanahewa kinaendelea na uchunguzi kubaini kama kuna mabaki hayo ya uhakika ni ya ndege hiyo, iliyopoteza mawasiliano Jumatatu saa 12.00 jioni, muda mfupi baada ya kuruka kutoka mji wa Punta Arenas.

Kikosi cha Jeshi la Wanahewa, kilitoa ramani ya njia iliyofuatwa ndege na muda wake kwamba ilitarajia kutua saa moja na dakika 17 katika kambi hiyo ya Eduardo Frei Montalva.

Kazi ya kusaka angani na baharini ilianza muda mfupi baada ya ndege kutoweka na tayari mataifa ya Argentina, Brazil, Uingereza na Uruguay, yameshatuma ndege kusaidia utafutaji wa ndege katika maji hayo ya barafu, huku Marekani na Israel zikitoa picha za setelaiti.

Abiria wa ndege hiyo, watatu walikuwa wanajeshi wa Chile, kati yao wawili ni wenye vyeo vya Meja Jenerali na Luteni Kanali na raia wawili walioajiriwa na kampuni ya uhandisi na ujenzi Inproser.

Wa tatu askari ni mwanamke pekee, Claudio Manzo (37), aliyejiunga na wanahewa mwaka 2008 na alipendelea kusafiri kwa ndege kufanya uchunguzi ardhini, kwa lengo la kupata habari kutoka maeneo yalio mbali.

Walikuwa wanaelekea kufanya kazi katika kambi hiyo ya kijeshi. Pia, kulikuwapo mwanafunzi na abiria 15 wa wanahewa, akiwamo kijana Ignacio Parada (24), aliyetambuliwa kutoka chuoni kwake ‘mwanafunzi bora.’

Alikuwa akisomea uhandisi katika Chuo Kikuu cha Magallanesna na katika safari hiyo alikuwa anaelekea katika kambi ya Antarctic kwa mafgunzo ya vitendo.

Pia, mfanyakazi wa kampuni ya Inproser, Leonel Cabrera na Jacob Pizarro, walikuwa wakielekea huko kufanya kazi katika kambi hiyo ya kijeshi.

Habari Kubwa