Umeme kuipaisha Wilaya Tanganyika

17Sep 2020
Neema Hussein
Katavi
Nipashe
Umeme kuipaisha Wilaya Tanganyika

MKUU wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Saleh Mhando, amesema mpango wa serikali kupeleka huduma ya umeme katika kila kijiji wilayani humo utasaidia kuboresha hali ya maisha kwa wananchi na kuchochea kukua kwa uchumi wa wilaya hiyo.

Mhando alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati wa ziara yake katika vijiji vya Mwese, Lugonesia na Lwege kukagua na kuhimiza shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wananchi.

Alisisitiza kuwa serikali imekusudia kupeleka huduma ya umeme kwa kila mwananchi pamoja na taasisi za umma kama shule, zahanati, masoko, nyumba za ibada, vituo vya polisi na ofisi nyingine za serikali ili kurahisisha na kuchochea utoaji huduma bora kwa wananchi. 

Aidha, aliwaeleza wananchi kwamba mradi wa umeme vijijini (REA) hauna fedha za kulipa fidia kwa mazao yatakayokatwa kupisha mradi huo na kuwataka wananchi kufanya maandalizi ya kupokea umeme huo.

Habari Kubwa