Utotoleshaji vifaranga samaki kuanza

08Jul 2020
WAANDISHI WETU
Dar es Salaam
Nipashe
Utotoleshaji vifaranga samaki kuanza

SERIKALI imesema mradi wa kutotolesha vifaranga vya samaki kwa ajili ya kukidhi soko nchini utaanza hivi karibuni ili kuchochea uchumi wa viwanda.

Mradi huo ni wa usimamizi wa uvuvi wa Kanda ya Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SwioFish), utakaotekelezwa Oktoba, mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi, Rashid Tamatamah, alipotembelea maonyesho ya Sabasaba.

"Mradi kama huu utasaidia kukuza sekta ya viwanda na uvuvi na kutoa elimu kwa wanafunzi ambao watapata fursa ya kujifunza kwa vitendo," alisema Tamatamah.

Alisema mchakato wa ujenzi wa mradi wa maabara ya vifaranga vya samaki Kunduchi umeanza na watashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baada ya miezi mitatu ujenzi utaanza kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Kadhalika, alisema katika maonyesho ya Sabasaba ya mwaka huu, watatoa elimu kwa wavuvi ya kuvua samaki wa kuliwa.

Habari Kubwa