720 wanufaika simu ‘Jaza Ujazwe’

09Sep 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
720 wanufaika simu ‘Jaza Ujazwe’

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, imetoa zawadi za simu papaso aina ya Tecno S1 kwa wateja wake 720 ambao wameshinda kupitia promosheni iliyofikia tamati ya ‘Jaza Ujazwe, Ujaziwe Zaidi’.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (), akikabidhi simu aina ya Tecno S1 kwa mmoja kati ya washindi 120, walioibuka washindi katika promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, Goodluck Mayanja.

Akizungumza kwenye hafla ya kutoa zawadi kwa washindi 120 kutoka Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Woinde Shisael, alisema wiki hii ni ya nne na ya mwisho katika utoaji wa zawadi.

“Tofauti na promosheni nyingine ambayo wateja wachache tu wanapata zawadi, Tigo inatoa simu moja ya Tecno S1, kila saa kwa masaa 24, kila siku ya wiki kwa muda wote wa kampeni hii. Kwa leo tumemalizia maana tumekabidhi simu zote 720,” alisema Shisael.

Shisael alisema promosheni hiyo inamuwezesha kila mteja wa Tigo kuwa na nafasi ya kujishindia simu anapoongeza salio na kupata zawadi za papo hapo za kifurushi cha muda wa hewani na kifurushi cha ujumbe mfupi kila anapoongeza salio.

“Tunafurahia kuona kwamba tumekuwa sehemu ya safari ya wateja wetu ambao wamejishindia simu za smartphone aina ya Tecno S1 ambao pia watafurahia mawasiliano ya bure ya simu kwa mwaka mmoja.

Zawadi nyingine ambazo mteja alikuwa anaweza kujishindia ni pamoja na bonasi ya bure kwenye huduma ya sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno SMS kulingana na matumizi ya mteja husika," aliongeza.

Kwa mujibu wa Tigo, simu hizo zitawawezesha washindi kupata taarifa mabalimbali, kuchukua picha na pia kuzitumia katika matumizi mbalimbali.

Habari Kubwa