Agizo mapato ya soko kulipiwa benki


10Jan 2020
Rahma Suleiman
Zanzibar
Nipashe
Agizo mapato ya soko kulipiwa benki


WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji Wanawake na Watoto, Maudline Cyrus Castico, 
ameliagiza Baraza la Manispaa Mjini Zanzibar kuhakikisha kuwa mapato 
yote yatayokusanywa katika soko la machinjio ya kuku Darajani kuwa
yatalipiwa benki.

WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji Wanawake na Watoto, Maudline Cyrus Castico, picha mtandao
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa soko jipya la kisasa la kuku
huko Darajani, alisema manispaa ina mambo mengi ya kufanya kazi hiyo ikiwamo
kuweka mji katika hali ya usafi, kujenga majengo mapya na ya kisasa na masuala
mengine, hivyo utunzaji wa fedha uzingatiwe kuepuka uvujaji ili malengo ya manispaa yafikiwe.


“Mpunguze kutegemea hazina, ujenge utamaduni malipo ya pesa
za soko la kuku mlipie benki,” alisema Waziri Castico.Alisema malengo yao yatatimia iwapo pale malipo ya kodi na makusanyo
mengine yatalipiwa moja kwa moja benki kwani ndiko kwenye dhamana ya
utunzaji wa fedha za serikali na mashirika.Aidha, waziri huyo aliliambia baraza hilo kuwa kwa kazi nyingine za manispaa
waingie ubia na watu kwani kufanya hivyo ni kutoa fursa ambazo zinahitajika na kulifanya baraza
lijiendeshe lenyewe.Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Idara Maluum za
SMZ, Shamata Ame, alilitaka Baraza la Manispaa kufanya kazi ipasavyo ili
juhudi zao ziweze kutambuliwa na kuthaminiwa.Alisema serikali itahakikisha masoko yote yatatengenezwa katika
mifumo inayokubalika duniani bila ya kuangalia maeneo au mahali yalipo.
 Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Mjini, Said Juma Ahmada, alisema wameandaa mikakati ya kuhakikisha mapato
yanapatikana katika soko hilo.Habari Kubwa