Bandari Mtwara yapigiwa chapuo

08Nov 2019
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe
Bandari Mtwara yapigiwa chapuo

SERIKALI imeiagiza Bodi ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) hadi kufikia Desemba, mwaka huu, ianze kuingiza mafuta

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, picha mtandao

Waziri Kalemani pia aliiagiza bodi hiyo kuhakikisha uwezo kwa ajili ya kusafirisha nchi jirani kupitia Bandari ya Mtwara.

Aidha, serikali imeitaka bodi hiyo kuhakikisha inawachukulia hatua kali ikiwamo kufungia kituo cha mafuta ambacho kitaficha mafuta kwa kutegea upandaji wa bei.

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, alisema hayo jana wakati wa kuzindua bodi mpya ya PBPA, jijini hapa.

Dk. Kalemani alisema hatua ya kuanza kutumia Bandari ya Mtwara kuingizia mafuta ya kusafirisha nchi jirani itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato.

"Naomba hakikisheni Bandari ya Mtwara nayo inaanza kuingiza mafuta ya kusafirishwa nchi za nje ili kuongeza mapato ya serikali. Kwa sasa tunapokea mafuta ya petroli na dezeli peke yake, hivyo ni lazima ifikapo Desemba, mwaka huu, tuanze kupokea na mafuta mengine ya kwenda nchi jirani za Malawi, Msumbiji na Zambia na taarifa niipate," alisema.

wa kuhifadhi mafuta katika Bandari ya Mtwara unaongezeka kutoka lita milioni 26 za sasa hadi milioni 80 kwa ajili ya mafuta ya mikoa ya Lindi na Mtwara na nchi jirani.

Alisema bodi hiyo inapaswa kuhakikisha inasimamia na kukomesha tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa vituo vya mafuta wanaoficha mafuta wakisubiri kupanda bei, alisema wafanyabiashara watakaobainika kufanya hivyo wachukuliwe hatua kali ikiwamo kufungiwa kituo.

"Wiki iliyopita bei ya mafuta haikupanda, kulikuwa na dalili za wafanyabiashara wengi kuanza kuficha mafuta wakisubiri bei ya mafuta ipande waanze kuuza, suala hilo halikubaliki," alisema Dk. Kalemani.

Habari Kubwa