Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Barcalys Tanzania, Kihara Maina, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Maina alisema taarifa za benki hiyo kusitisha huduma zake zilikuwapo, lakini baada ya kutoka kwa taarifa ya mwaka wa fedha, Barclays itaendelea kufanya kazi kama kawaida.
“Napenda kuwaambia Watanzania kuwa tutaendelea kutoa huduma zetu kama kawaida tena mara mbili ya hapo awali, wale wote walioweka fedha zao Barclays waondoe hofu ziko salama, wafahamu kuwa hatutafunga benki hii,” alisema.
Maina alisema wafanyakazi 500 wa benki hiyo nchini, wataendelea kufanya kazi kama kawaida na wapo katika mpango wa kuwashawishi kuendelea kubaki baada ya taarifa hiyo kutoka.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Afrika, Maria Ramos, alisema Barclays bado ipo imara na itaendelea kutoa huduma zake kwa sababu ina matawi mengi.