Bei ya mahindi mwaka huu yatajwa

23May 2020
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Bei ya mahindi mwaka huu yatajwa

SERIKALI imesema bei za mahindi kwa mwaka huu sokoni zimeanzia Sh. 500 mpaka Sh. 800 kwa kilo moja ya mahindi.

Hayo yalibainishwa jana na Wizara ya Kilimo ilipokuwa ikijibu swali la Mbunge wa Kwela (CCM), Ignas Malocha.

Katika swali lake, mbunge huyo alisema serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeshusha bei ya kununua mahindi toka bei ya kilo moja kwa Sh.500 mpaka Sh.380 kwa kilo.

"Je, ni sababu zipi zimepelekea serikali kupunguza bei ya mahindi badala ya kuongeza na je, serikali inaweza kuwaelekeza wakulima gharama ya kuzalisha kilo moja ya mahindi toka kuandaa shamba, kulima, kupanda, kuvuna mpaka kufikisha sokoni?" Alihoji.

Katika majibu ya wizara hiyo ilisema bei ya mazao hupangwa na nguvu ya soko na serikali kupitia wakala haijashusha bei ya mahindi.

"Bei zimekuwa zikibadilika kwa kuzingatia bei za soko wakati wa ununuzi wa mahindi, ambapo katika msimu wa ununuzi 2019/20 wakala umenunua nafaka kwa bei Sh.500 had

Habari Kubwa