Benki ya posta yazindua huduma za kibenki Babati

10Feb 2016
Babati, Arusha
Nipashe
Benki ya posta yazindua huduma za kibenki Babati

BENKI ya Posta Tanzania (TPB), imezindua huduma za kibenki kwa kufungua tawi lake jipya kwenye mji wa Babati mkoani Manyara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Prof. Lettice Rutashobya.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Prof. Lettice Rutashobya, alisema tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.

“Tawi hili limefunguliwa ili kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake,” Prof. Rutashobya.

Aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati kwa kutumia huduma za benki hiyo na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya matawi yanayofanya vizuri kifaida.

Naye Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za kibenki za tawi hilo, aliipongeza benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya kuninua maisha ya Mtanzania wa hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki karibu na wananchi na kwa kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo ya masharti nafuu.

Mafuru aliwashauri wakazi wa Babati kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba mikopo ambayo inatolewa kwa riba nafuu.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, alisema: “Azma ya Benki ya Posta, ni kuwafikia na kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote.