Bilioni 28/- kusambaza umeme maeneo mapya

18Jan 2021
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Bilioni 28/- kusambaza umeme maeneo mapya

SHIRIKA la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, linatarajia kutumia Sh. bilioni 27.7 kusambaza umeme kuyafikia maeneo mapya yanayokua kwa kasi ndani ya Jiji la Dodoma.

Meneja wa shirika hilo mkoani hapa, Frank Chambua, aliyasema hayo jana katika kikao kilichowakutanisha wakuu wa taasisi za kiserikali za jiji hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, alikuwa akipokea taarifa ya mipango ya upelekaji huduma kwenye maeneo ya uwekezaji na yanayojengwa kwa kasi jijini hapa.

Alisema shirika limejipanga kujenga miradi hiyo mipya ya kuunganisha wateja kwenye maeneo yanayokua kwa kasi.

Meneja huyo alisema mipango ya muda mfupi ya shirika ni kujenga miradi mipya ya kimkakati itakayogharimu Sh. bilioni 3.3 ikiwamo eneo la viwanda la Nala.

“Katika ziara yetu tuliyofanya na Mkuu wa Mkoa mwishoni mwa mwaka jana, kuna baadhi ya maeneo tulipita na yakaainishwa ili yatengenezewe mkakati wa kupeleka umeme kwenye maeneo hayo, mojawapo ni Nala.

"Tumefanya tathmini na kubaini kwamba kupeleka umeme pale zinahitajika Sh. milioni 678, mradi bado haujaanza tupo kwenye harakati za kutafuta fedha," alisema.

Alisema katika eneo la viwanda Nala zinahitajika Sh. bilioni 1.5, Mahungu Sh. milioni 695 na eneo la Iyumbu jirani na shule ya mfano zinahitajika Sh. milioni 188.

“Eneo lingine ni Michese ambako zinahitajika Sh. milioni 168, tumepata Sh. milioni 25, eneo la Mkalama zinahitajika Sh. milioni 84 na tayari tumepata Sh. milioni 11 mradi unaendelea.

"Upanuzi wa kituo cha Zuzu umekamilika, umegharimu Dola za Marekani milioni 53, kuna mpango wa ujenzi wa njia nane za umeme za msongo wa kilovolti 33 kupeleka maeneo tofauti zenye jumla ya urefu wa kilomita 153.9 zinazokadiriwa kugharimu Sh. bilioni 9.3," alisema...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa