Brela yafunguka mwamko mzuri wa biashara kaskazini

12Jun 2019
Mary Mosha
MOSHI
Nipashe
Brela yafunguka mwamko mzuri wa biashara kaskazini

WAKALA  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)  umesema  mwamko wa urasimishaji wa biashara kwa mikoa minne ya kanda ya kaskazini umepata mjongeo chanya ikilinganishwa na  kanda nyingine nchini.

Mkurugenzi wa Utawala  na Fedha wa Brela,  Bakari  Mketo.

Kasi ya usajili wa kampuni kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga inaongeza hamasa kitaifa, licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto ya  ukosefu wa elimu ya namna bora ya kujisajili kupitia njia yamtandao.

Mkurugenzi wa Utawala  na Fedha wa Brela,  Bakari  Mketo, aliyasema hayo jana, wakati wa utoaji elimu ya mafunzo  ya namna bora ya  kutumia mtandao  katika zoezi la urasimishaji wa biashara kwa wamiliki wa kampuni mbalimbali.Mketo alisema  licha ya kuwapo kwa ofisi zao katika kanda  mbalimbali hapa nchini,  lakini  tumekuwa tukipokea  simu nyingi  kutoka   kanda ya Kaskazini hasa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wanaotakakurasimisha  biashara zao ili kuweza kutambulika kisheria.“Tulipotoa maoni kutoka kwa wananchi ya kutaka kuweka ofisi  kila  mkoa, lakini  tumeona bado haitasaidia kuwafikia wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini na badala yake tukaamua kuongeza nguvu kwenyenamna ya  kutumia mtandao kurasimisha  biashara,  ili  wananchi  waweze kuendana na wakati  na kuongeza ushindani wa kimataifa,” alisema. “Tunachotoa hasa mbali na elimu  ya namna bora ya kutumia mtandao kujisajili  pia  tunawaeleza  umuhimu wa urasimishaji wa biashara zao, ili waweze kutambulika  maeneo mbalimbali ikiwamo taasisi za kifedha,  ushindani wa zabuni  serikalini  pamoja na  kulalamika ikiwa mtu ametumia  jina la kamapuni/biashara  yako,” alisema.Alisema gharama za usajili zinatofautiana kulingana na aina ya usajili husika  kwa kampuni ambazo ni kati ya Sh. 175,000 hadi 512,200 kwa kiwango cha juu kwa  kampuni,  ingawa usajili huo unategemea na mtaji uliopo kwenye mkataba wa makubaliano (MoU).Pamoja na mambo mengine, Ofisa wa  Brela kutoka Kitengo cha Miliki Bunifu, Suzana Senso, alisema kwa kasi ya nchi yetu na dunia kwa ujumla ni kwamba urasimishaji wa biashara haukwepeki, hivyo wajasiriamali wote wanapaswa kusajili biashara zao kabla ya kuanza kijitangaza  kwa kiwango kikubwa na baadaye kupata hasara  kwani  wapo wanaowahi   kufanya usajili  kwa majina hayo.

“Tunawaomba wafanyabiashara kabla ya kuanza kuzitangaza biashara zao wafike ofisini kwetu   kwa ajili ya urasimishaji kwani wengi wamekuwa wakipata hasara baada ya kutumia jina  kuzitangaza biashara zao na wanapofika kwetu wanakuta jina hilo tayari linatumika na mtu mwengine,” alisema. 

“Tupo  hapa mkoani Kilimanjaro kwa siku  tatu ambapo tutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu  ya namna bora  kutumia mtandao  pia   tutafanya ukaguzi, na  kufanyia kazi changamoto  tulizoziona, ambapo panamkanganyiko  wa nani ni mrasimishaji wa biashara kwani wapo ambao wanakwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).”

Habari Kubwa