Fursa uchumi viwanda yahimizwa

28Mar 2018
Ibrahim Yassin
MOMBA
Nipashe
Fursa uchumi viwanda yahimizwa

KATIBU wa Siasa na Mambo ya Nje wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ngemela Lubinga, amewataka wananchi wilayani Momba mkoani Songwe kuchangamkia fursa za viwanda ili kujikwamua na umaskini kwa kuwa kaulimbiu ya serikali ya sasa ni uchumi wa viwanda.

KATIBU wa Siasa na Mambo ya Nje wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ngemela Lubinga.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati akitembelea kiwanda cha kuzalisha chumvi kilichopo Kata ya Ivuna ambapo alisema mradi huo ukitumiwa vizuri utainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na serikali kwa ujumla.

 

Lubinga alishauri wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) washirikishwe katika uchumi wa viwanda, ili waweze kujikwamua kiuchumi.

 

Mkuu wa wilaya hiyo, Juma Irando, alisema wamepokea maagizo ya chama, na kueleza kuwa serikali imejipanga kujenga viwanda na kuongeza ajira kwa wananchi, hivyo ana uhakika kiwanda hicho kitatoa ajira kwa wananchi na kuongeza fursa za kiuchumi.

 

Twaha Maulid, Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa, alisema uchumi wa viwanda ni sera ya chama hicho,na kuwa chama hicho kitahakikisha kinaisimamia serikali katika kufanikisha uzalishaji na ajira kwenye kiwanda hicho vi na vingine.

 

Stella Kandonga, mkazi wa Ivuna, alisema wamepata faraja kuona jinsi chumvi ilivyokuwa nyingi kwenye mgodi huo uliopo kwenye kijiji chao ambapo wananchi wamepewa kipaumbele cha kuzalisha.

 

Kandonga alishauri kwamba ili wananchi wote wanufaike, masuala ya itikadi za kisiasa yawekwe pembeni.

 

 

 

Habari Kubwa