Halmashauri yabaini shida machinga stendi ya mabasi

13Jan 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Halmashauri yabaini shida machinga stendi ya mabasi

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imemwagiza Meneja wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma, kuweka utaratibu mzuri kwa ajili ya wajasiriamali kufanya shughuli zao kituoni huko.

Agizo hilo lilitolewa jana na Meya wa Jiji hilo, Profesa Davis Mwamfupe, alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kujionea hali ya huduma.

Profesa Mwamfupe alisema amebaini kuwapo mrundikano wa bidhaa katika eneo la kituo hicho, jambo ambalo linapaswa kuwekewa utaratibu.

Alimtaka meneja wa kituo hicho kuweka utaratibu mzuri kwa ajili wajasiriamali kutokana na kufanya biashara kwenye kumbi za abiria.

“Kuna mrundikano wa bidhaa za wajasiriamali katika maeneo mbalimbali kituoni hapa, hasa katika kumbi za kukaa na kusubiria mabasi abiria na bidhaa zilizoenea katika njia zilizotengwa kwa ajili ya abiria kupita ni tatizo,” alisema.

Mmoja wa abiria waliozungumza na Nipashe kituoni huko, Juliana Nyoni, alisema utaratibu mzuri unatakiwa kuandaliwa ili abiria wasipate bugudha na kulinda usalama wa mali zao....soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa